Taarifa mpya kuhusu COVID-19: Queensland yatoa mwelekeo wayo wa 80% kwa kufunguliwa

Hii ni taarifa mpya kuhusu Coronavirus nchini Australia kwa 9 Novemba 2021.

Kiongozi wa Queensland Annastacia Palaszczuk (katikati) akizungumza na wafanyakazi katika kituo cha chanjo cha Logan

Kiongozi wa Queensland Annastacia Palaszczuk (katikati), akizungumza na wafanyakazi katika kituo cha chanjo cha Logan. Source: AAP Image/Jono Searle

Mambo Mhimu

  • Queensland yatangaza hatua kadhaa kwa watu ambao wame pata chanjo kamili.
  • Kuanzia 17 Disemba, au wakati jimbo hilo litafikisha 80% ya utoaji wa chanjo mbili, hapatakuwa vizuizi vya COVID-19 kwa mabaa na sehemu zingine za burudani, viwanja vya michezo na kadhalika.

  • Watu ambao wame chanjwa ndiwo watakao ruhusiwa tu kutembelea hospitali, msamaha wapekee utakuwa tu kwa hali za mwisho wa maisha au hali za dharura.
  • Haitakuwa lazima kwa watu wa Queensland kuvaa barakoa isipokuwa wakati wakusafiri kwa ndege, na ndani ya viwanja vya ndege punde jimbo hilo litakapo timiza lengo la 80% ya chanjo ya kwanza.
  • Ripoti mpya kutoka taasisi ya Doherty imepata kuwa ufunikaji wa chanjo ya UVIKO-19, ni zaidi ya 70% na takriban nusu ya maambukizi yote yatakuwa miongoni mwa watu walio chanjwa, ila katika viwango vidogo na katika hali ndogo ya uambukizi.
  • Chini ya mpango wa hatua 3 wakufungua jimbo, Wilaya ya Kaskazini ita anza mpango wa karantini ya nyumbani kuanzia 23 Novemba.

Kesi za UVIKO-19:

  • Victoria imerekodi kesi mpya 1,069 za maambukizi pamoja na vifo 10.
  • NSW imerekodi kesi mpya 222 pamoja na vifo 4.


Karantini, safari, zahanati za vipimo na malipo ya janga

Karantini na masharti yavipimo husimamiwa nakutekelezwa na serikali zamajimbo na wilaya:

ACT Usafiri na Karantini
Kama unataka safiri ng'ambo, unaweza omba kibali mtandaoni. Bonyeza hapa kwa taarifa zaidi kuhusu masharti yakuondoka Australia. Kuna hatua za mpito kwa safari zakimataifa ambazo hutathminiwa mara kwa mara na serikali, nakuchapishwa kwenye tovuti ya Smart Traveller.



Tazama rasilmali zilizo tafsiriwa za huduma yamawasiliano ya shirika la afya ya tamaduni nyingi ya NSW:


Zahanati za vipimo katika kila jimbo na wilaya:

NSW 
ACT 

Taarifa kuhusu malipo ya janga katika kila jimbo la wilaya:

NSW 
ACT 

Share

Published

Updated

By SBS/ALC Content
Presented by Gode Migerano
Source: SBS

Share this with family and friends


Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service