Taarif mpya kuhusu COVID-19: Vizuizi kuregezwa katika sehemu za hatari za COVID jimboni NSW, Victoria yatangaza mwelekeo wakuondoka katika amri yakufungiwa ndani

Hii ni taarifa mpya kuhusu Coronavirus nchini Australia kwa tarehe 19 Septemba 2021.

VIC CORONAVIRUS COVID19

Watu wachangia chakula katika eneo la Albert Park Lake mjini Melbourne, Jumapili, Septemba 19, 2021. Source: AAP/DANIEL POCKETT

 

  • Kiongozi wa NSW atangaza kuregezwa kwa vizuizi katika halmashauri za jiji zenye wasi wasi.
  • Victoria yatoa mwongozo wakufungua jimbo tena
  • ACT yaripoti kesi mpya 17 za COVID-19 ndani ya jamii
  • Queensland yaweka rekodi mpya ya chanjo nyingi zaidi katika siku moja
 


 

New South Wales
 

NSW imerekodi kesi mpya 1,083 za maambukizi ndani ya jamii, pamoja na vifo 13.

 

Kiongozi wa jimbo hilo Gladys Berejiklian alitangaza kuwa kuanzia Jumatatu 20 Septemba, sehemu zote za wasiwasi zitakuwa na sheria sawia na eneo lote la Greater Sydney, ila masharti yawafanyakazi wanao ruhusiwa pamoja na masharti ya vibali vya usafiri vitasalia.

 

Sehemu za kuogoela za nje kote jimboni NSW, zitafunguliwa kuanzia Jumatatu 27 Septemba, kama zitakuwa na mpango salama wa COVID unao idhinishwa.

Kwa sasa 81.9% ya wakaaji wa NSW wanao stahiki, wamepokea dozi ya kwanza ya chanjo na 51.9% ya wakaaji wame pokea chanjo kamili. 

 

Bonyeza hapa kuomba miadi yako ya chanjo leo. 

Victoria

 

Victoria imerekodi kesi mpya 507 ndani ya jamii, pamoja na kifo kimoja.

 

Kiongozi wa jimbo hilo Daniel Andrews aliweka wazi mchakato wenye hatua tano zakuondoa jimbo hilo ndani ya vizuizi. Makatazo yata isha wakati 70% ya umma wa jimbo hilo wanao stahiki wame pata chanjo kamili, hatua ambayo inatarajiwa itakamilika tarehe 26 Oktoba. “Tuna fungua tena, na hapatakuwa kurudi nyuma” Bw Andrews alisema. Kufikia siku ya krismasi, idadi ya wageni 30 wata ruhusiwa ndani ya nyumba moja, kama viwango vya 80% vya chanjo vina timizwa.

 

Data inaonesha angalau 71.2% ya watu wa Victoria wanao stahiki, wamepokea angalau dozi moja ya chanjo ya COVID-19 na, 43.5% yao wame pokea chanjo kamili.

 

Pata hapa kituo cha chanjo kilicho karibu yako.

 

Hali ilivyokuwa nchini Australia katika masaa 24
 

  • ACT imerekodi kesi mpya 17 za maambukizi, 12 kati yazo zilikuwa katika hali ambukizi ndani ya jamii kwa muda.
  • Idadi ya watu 31,004 wa Queensland walichanjwa jana, hiyo ikiwa ni rekodi kwa jimbo hilo. 59.34% yawatu kwa sasa wame pata tayari dozi yao ya kwanza.

Karantini, safari, zahanati za vipimo na malipo ya janga
Karantini na masharti yavipimo husimamiwa nakutekelezwa na serikali zamajimbo na wilaya:

ACT Usafiri na Karantini
Kama unataka safiri ng'ambo, unaweza omba kibali mtandaoni. Bonyeza hapa kwa taarifa zaidi kuhusu masharti yakuondoka Australia. Kuna hatua za mpito kwa safari zakimataifa ambazo hutathminiwa mara kwa mara na serikali, nakuchapishwa kwenye tovuti ya Smart Traveller.



Tazama rasilmali zilizo tafsiriwa za huduma yamawasiliano ya shirika la afya ya tamaduni nyingi ya NSW:


Zahanati za vipimo katika kila jimbo na wilaya:

NSW 
ACT 

Taarifa kuhusu malipo ya janga katika kila jimbo la wilaya:

NSW 
ACT 

Share

Published

By SBS/ALC Content
Presented by Gode Migerano
Source: SBS

Share this with family and friends


Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service
Taarif mpya kuhusu COVID-19: Vizuizi kuregezwa katika sehemu za hatari za COVID jimboni NSW, Victoria yatangaza mwelekeo wakuondoka katika amri yakufungiwa ndani | SBS Swahili