Taarifa mpya kuhusu COVID-19: Majimbo yatangaza mifuko yakiuchumi wakati NSW na Victoria zarekodi kesi chache za covid

Hii ni taarifa mpya kuhusu Coronavirus nchini Australia kwa 12 Oktoba 2021.

Kiongozi wa Victoria Daniel Andrews azungumza na vyombo vya habari mjini Melbourne

Kiongozi wa Victoria Daniel Andrews azungumza na vyombo vya habari mjini Melbourne. Source: AAP Image/James Ross

  • NSW yatangaza mfuko wa uponaji wa COVID-19 kwa biashara
  • Victoria kufanya uwekezaji mkubwa katika huduma ya afya
  • Serikali ya madola yatangaza inacho ita mpango wa kwanza wa dunia kwa ugonjwa wa akili katika watoto

Victoria

Victoria imerekodi kesi mpya 1,466 za maambukizi ya COVID-19 ndani ya jamii pamoja na vifo vinane. Miongoni mwa watu 675 ambao wako hospitalini, ni asilimia saba tu ndiwo walio pata chanjo kamili.

Kiongozi wa jimbo hilo Daniel Andrews amewahamasisha watu wa Victoria, waombe miadi yao ya chanjo ya pili isogezwe karibu zaidi kama inawezekana.

Jimbo hilo limetangaza uwekezaji wama milioni ya dola katika huduma ya afya kabla ya jimbo hilo kufunguliwa tena.

$255 milioni zimetangazwa kusaidia nguvu kazi ya mstari wa mbele wa COVID hospitalini, pamoja na $2.5 milioni zitakazo tengwa kuwaajiri wafanyakazi 1000 wa huduma ya afya wanao ishi ng'ambo.

New South Wales

New South Wales imerekodi kesi mpya 360 za covid ndani ya jamii pamoja na vifo vitano.

Kiongozi wa jimbo hilo Dominic Perrottet ametangaza mfuko wa biashara kwa jimbo hilo.

Wafanyabiashara wanao stahiki wataweza dai punguzo ya $2,000 kwa baadhi ya huduma na malipo. Mapunguzo makubwa yametangazwa kwa biashara, zenye bidhaa zinazo haribika haraka kabla ya msimu wa krismasi.

“Tunataka wamiliki wabiashara wajue kuwa tuna waunga mkono,” Bw. Perrottet alinukuliwa.

Jimbo hilo linatarajia kupita malengo ya 80% ya chanjo kamili kufikia jumatatu, takwimu hiyo itakuwa hatua nyingine yakuregeza vizuizi.

Pata hapa kituo cha chanjo kilicho karibu yako.

ACT

Wilaya ya ACT imerekodi kesi mpya 28, kesi 22 kati yazo zime ungwa na kesi zinazo julikana.

Bonyeza hapa kuomba miadi yako ya chanjo leo.

Hali ilivyokuwa nchini Australia katika masaa 24

  • Queensland haija rekodi kesi yoyote ya COVID-19.
  • 82.8% ya wakaaji wa Australia wamepokea dozi yao ya kwanza ya COVID, na 63.4% yao wame pata chanjo kamili.
  • Waziri wa Afya wa serikali ya madola Greg Hunt amesema ushauri kwa dozi za jeki kwa watu wazima, zitapatikana kabla ya mwisho wa Oktoba.

Karantini, safari, zahanati za vipimo na malipo ya janga

Karantini na masharti yavipimo husimamiwa nakutekelezwa na serikali zamajimbo na wilaya:

ACT Usafiri na Karantini
Kama unataka safiri ng'ambo, unaweza omba kibali mtandaoni. Bonyeza hapa kwa taarifa zaidi kuhusu masharti yakuondoka Australia. Kuna hatua za mpito kwa safari zakimataifa ambazo hutathminiwa mara kwa mara na serikali, nakuchapishwa kwenye tovuti ya Smart Traveller.



Tazama rasilmali zilizo tafsiriwa za huduma yamawasiliano ya shirika la afya ya tamaduni nyingi ya NSW:


Zahanati za vipimo katika kila jimbo na wilaya:

NSW 
ACT 

Taarifa kuhusu malipo ya janga katika kila jimbo la wilaya:

NSW 
ACT 

Share

Published

By SBS/ALC Content
Presented by Gode Migerano
Source: SBS

Share this with family and friends


Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service
Taarifa mpya kuhusu COVID-19: Majimbo yatangaza mifuko yakiuchumi wakati NSW na Victoria zarekodi kesi chache za covid | SBS Swahili