Taarifa mpya kuhusu COVID-19: Sydney yafungua zahanati mpya za chanjo bila miadi

Hii ni taarifa mpya kuhusu Coronavirus nchini Australia, kwa tarehe 27 Julai 2021.

Polisi waonekana nje ya jengo ambalo liko chini ya makatazo yakutoka, katika mtaa wa Devitt Street, katika kitongoji cha Magharibi Sydney cha Blacktown

Polisi waonekana nje ya jengo ambalo liko chini ya makatazo yakutoka, katika mtaa wa Devitt Street, katika kitongoji cha Magharibi Sydney cha Blacktown Source: AAP Image/Mick Tsikas

  • Zahanati za chanjo bila miadai, zafunguliwa Magharibi Sydney.
  • Victoria na Kusini Australia zamaliza makatazo usiku wa manane.
  • Hakuna kesi mpya Kusini Australia na Queensland.
  • Viwango vya chini vya chanjo miongoni mwa watu wenye zaidi ya miaka 60 vyazua wasiwasi.

New South Wales
New South Wales imerekodi kesi mpya 172 ndani ya jamii, kesi 60 ndani ya jamii zikiwa katika hali ambukizi. Jengo moja katika kitongoji cha Blacktown kiko chini ya ulinzi wa jeshi la polisi, baada ya vipimo vya wakaaji sita kurejesha matokeo chanya ya COVID-19.

Idara ya Afya ya NSW imetoa chanjo za COVID-19 za AstraZeneca, kwa wanachama wote wa jamii wenye zaidi ya miaka 40 na zaidi katika zahanati bila miadi katika vitongoji vya Merrylands na Guilford ambavyo viko Magharibi Sydney.

Kuanzia kesho, watu wenye zaidi ya miaka 18 wanaweza pata chanjo ya COVID-19 ya AstraZeneca, kutoka duka za madawa, amesema kiongozi wa NSW Gladys Berejiklian ambaye amehamasisha kila mtu apokee chanjo haraka iwezekanavyo.

Victoria
Victoria imerekodi kesi mpya 10 ndani ya jamii, zote zilikuwa ndani ya karantini katika hali ambukizi. Makatazo ya tano yanatarajiwa kuisha saa tano dakika hamsini na tisa usiku wa leo kwa masaa ya mashariki Australia ila, baadhi ya vizuizi vita salia kwa wiki zingine mbili.

Wakaaji wa Victoria hawa ruhusiwi kuwapokea wageni nyumbani, mikusanyiko ya umma inakikomo cha watu 10 na, ni lazima kuendelea kuvaa barakao. Pata hapa taarifa mpya kuhusu vizuizi vya COVID-19.

Hali ilivyo kuwa nchini Australia katika masaa 24 yaliyo pita
  • Maeneo ya Wagga Wagga, Hay, Lockhart na Murrumbidgee haya jumuishwi tena katika mpango wa mpaka kati ya Victoria na NSW.
  • Ni 15% tu yawatu wenye zaidi ya miaka 60, ndiwo wamepokea chanjo kamili, kulingana na data za serikali yamadola.



Karantini, usafiri, zahanati za vipimo na malipo ya janga

Masharti ya Karantini na vipimo, yana simamiwa nakutekelezwa na serikali za majimbo na mikoa:


ACT Usafiri na Karantini
Kama unataka safiri ng'ambo, unaweza wasilisha ombi lako mtandoani kupewa ruhusa. Bonyeza hapa kwa taarifa zaidi kuhusu masharti yakuondoka Australia. Kuna hatua za mpito kwa safari zakimataifa ambazo, hutathminiwa mara kwa mara na serikali na taarifa mpya huchapishwa kwenye tovuti ya Smart Traveller.





Tazama rasilimali zilizo tafsiriwa nakuchapishwa na huduma ya mawasiliano ya afya NSW Multicultural Health:


Zahanati za vipimo katika kila jimbo na mkoa:


NSW 
ACT 

Taarifa kuhusu malipo ya janga katika kila jimbo na mkoa:

NSW 
ACT 

Share

Published

Updated

By SBS/ALC Content, Gode Migerano
Presented by Gode Migerano
Source: SBS

Share this with family and friends


Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service