Taarifa mpya ya COVID-19: Vifo viwili vipya vya COVID-19 vya rekodiwa NSW

Hii ni taarifa mpya kuhusu Coronavirus nchini Australia ya 25 Julai 2021.

Kiongozi wa NSW Gladys Berejiklian atoa taarifa mpya kuhusu COVID-19 mjini Sydney.

Kiongozi wa NSW Gladys Berejiklian atoa taarifa mpya kuhusu COVID-19 mjini Sydney, Jumapili, 25 Julai, 2021. Source: AAP Image/Lisa Maree Williams

  • NSW yarekodi vifo viwili kutoka COVID-19.  
  • Kesi zote jimboni Victoria zina ungwa kwa mlipuko wa sasa. 
  • Serikali ya Shirikisho yapata dozi milioni 85 za ziada za Pfizer.
  • Hatua zaku inua makatazo ya Kusini Australia zaendelea vizuri. 

New South Wales

NSW imerekodi kesi mpya 141 ndani ya jamii. Watu wawili wamefariki, mwamke mmoja katika miaka ya sabini, na mwanamke mmoja katika miaka ya 30 ambao hawakuwa na magonjwa sugu, kiongozi wa NSW Berejikilian amesema. 

NSW itapokea dozi za ziada za COVID-19 elfu 50,000 za Pfizer. Wakati huo huo, kitengo maalum cha polisi kime undwa kuwatambua watu walio shiriki katika maandamano ya jana, hati za adhabu 510 zikiwa zimetolewa tayari.

Pata hapa sehemu ambako kesi ziko katika orodha au ramani.

Victoria

Victoria imerekodi kesi mpya 11 ndani ya jamii, zote zilikuwa ndani ya karantini katika wakati wote ambao zilikuwa katika hali ambukizi na, zina ungwa kwa mlipuko wa sasa.

Mamlaka bado hawaja thibitisha hatua zaku regezwa kwa vizuizi vya COVID-19 Jumanne 27 Julai 2021.

Pata hapa, sehemu ambako kesi ziko kwenye orodha au ramani.

Hali ilivyo kuwa nchini Australia katika masaa 24 yaliyo pita

  • Australia itapokea dozi za chanjo ya COVID-19 milioni 85 za Pfizer katika miaka ya 2022 na 2023.
  • Kusini Australia imerekodi kesi mpya tatu ndani ya jamii, na bado jimbo hilo liko katika mwelekeo waku inua makatazo.  
  • Queensland imerekodi kesi mpya tano ndani ya karantini ya hoteli.

Taarifa potovu kuhusu COVID-19:
Vijana wenye afya nzuri hawa athiriwi na COVID-19. Ina waathiri nakuwaua tu wazee au wagonjwa.

Ukweli kuhusu COVID-19:
Virusi hivyo huwa athiri wazee na wale ambao wana magonjwa sugu zaidi ila pia, vina waathiri nakuwaua baadhi ya vijana ambao wana afya nzuri.


Karantini, usafiri, zahanati za vipimo na malipo ya janga

Masharti ya karantini na vipimo yana simamiwa na kutekelezwa na serikali za majimbo na mikoa:


ACT Usafiri na Karantini
QLD Usafiri na Karantini
TAS Usafiri na Karantini
Kama unataka safiri ng'ambo, unaweza wasilisha ombi lako mtandaoni. Bonyeza hapa kwa taarifa zaidi kuhusu masharti yakuondoka Australia.

 

Kuna hatua za mpito kwa safari zakimataifa ambazo, huwa zina tathminiwa kila mara na serikali na, taarifa mpya kuchapishwa kwenye tovuti ya Smart Traveller.





Tembelea shirika la NSW Multicultural Health Communication Service kwa huduma zilizo tafsiriwa:

Zahanati za vipimo katika kila jimbo na mkoa:


NSW 
ACT 

Taarifa kuhusu malipo ya janga katika kila jimbo na mkoa:

NSW 
ACT 

Share

Published

Updated

By Gode Migerano, SBS/ALC Content
Presented by SBS/ALC Content, Gode Migerano
Source: SBS

Share this with family and friends


Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service