Taarifa mpya kuhusu COVID-19: Victoria yaweka rekodi yakitaifa kwa idadi ya maambukizi yakila siku

Hii ni taarifa mpya kuhusu Coronavirus nchini Australia kwa 5 Oktoba 2021.

Watu wajaa ndani ya jengo lakifalme la maonesho ambako chanjo za COVID-19 zatolewa mjini Melbourne

Watu wajaa ndani ya jengo lakifalme la maonesho ambako chanjo za COVID-19 zatolewa mjini Melbourne Alhamisi, Septemba 2, 2021. Source: AAP Image/Daniel Pockett

  • Maelfu ya miadi ya chanjo ipo Victoria
  • Jimboni NSW, 67.5% yawatu wamepata chanjo kamili
  • Zaidi ya 94% ya wakaaji wa Canberra wenye zaidi ya miaka 12 wamepata chanjo moja
  • Queensland yarekodi kesi mbili mpya ndani ya jamii

Victoria

Victoria imerekodi kesi mpya 1,763 ndani ya jamii, idadi ambay imekuwa kubwa zaidi ya kila siku ya jimbo lolote na wilaya nchini Australia, tangu mwanzo wa janga. Watu wane wame fariki pia.

Kiongozi wa jimbo hilo Daniel Andrews amesema kuna maelfu ya miadi wa chanjo za Pfizer, AstraZeneca na Moderna.

Kuanzia leo, sekta ya ujenzi inafunguliwa ila ni wafanyakazi tu walio chanjwa ndiwo wataruhusiwa kurejea kazini, kama wanafuata miongozo mikali ya usalama ya COVID-19.

Kanda ya Latrobe Valley, itaondoka kutoka makatazo yakubaki ndani kuanzia usiku wa manane usiku wa leo.

Pata hapa kituo cha chanjo karibu yako.

New South Wales

NSW imerekodi kesi mpya 608 ndani ya jamii pamoja na vifo saba.

Idadi ya asilimia 88.5 ya watu wenye miaka 16 na zaidi wamepata dozi moja ya chanjo, wakati asilimia 67.5 wamepata chanjo kamili kufikia saa tano dakika 59 usiku wa Jumapili 3 Oktoba 2021.

Amri zakubaki nyumbani zimengezwa hadi tarehe 11 Oktoba katika miji ya Taree, Forster-Tuncurry na Muswellbrook kwa sababu ya ongezeko ya idadi ya kesi katika maeneo hayo. 

Bonyeza hapa kuomba miadi yako ya chanjo leo.

Australian Capital Territory

Wilaya hiyo imerekodi kesi mpya 33 ndani ya jamii, 14 kati yazo zilikuwa katika hali ambukizi ndani ya jamii.

Idadi ya asilimia 94 ya watu wenye miaka 12 na zaidi, wamepata dozi yao ya kwanza ya chanjo wakati, zaidi ya asiimia 65 yawatu wame pokea dozi yao ya pili ya chanjo.

Masaa 24 yaliyo pita nchini Australia

  • Australia kufikia kiwango cha 80% ya watu wenye zaidi ya miaka 16 ambao wame pata chanjo kamili, kufikia katikati ya mwezi wa Novemba.

Karantini, safari, zahanati za vipimo na malipo ya janga
Karantini na masharti yavipimo husimamiwa nakutekelezwa na serikali zamajimbo na wilaya:

ACT Usafiri na Karantini
Kama unataka safiri ng'ambo, unaweza omba kibali mtandaoni. Bonyeza hapa kwa taarifa zaidi kuhusu masharti yakuondoka Australia. Kuna hatua za mpito kwa safari zakimataifa ambazo hutathminiwa mara kwa mara na serikali, nakuchapishwa kwenye tovuti ya Smart Traveller.



Tazama rasilmali zilizo tafsiriwa za huduma yamawasiliano ya shirika la afya ya tamaduni nyingi ya NSW:


Zahanati za vipimo katika kila jimbo na wilaya:

NSW 
ACT 

Taarifa kuhusu malipo ya janga katika kila jimbo la wilaya:

NSW 
ACT 

Share

Published

By SBS/ALC Content
Presented by Gode Migerano
Source: SBS

Share this with family and friends


Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service