Taarifa mpya ya COVID-19: Polisi wa Victoria wakamata zaidi ya watu mia moja, NSW kupunguza muda wakujitenga

Hii ni taarifa mpya kuhusu Coronavirus nchini Australia kwa 3 Oktoba 2021.

Polisi wamkamata mwandamanaji MELBOURNE

Polisi wa Victoria wamkamata mwandamanaji karibu ya Royal Botanic Gardens, kwenye maandamano dhidi ya chanjo mjini Melbourne, Jumamosi, Oktoba 2, 2021. Source: AAP Image

  • Victoria yaripoti kesi mpya 1,220 ndani ya jamii
  • Mamlaka NSW wahamasisha wakaaji kufuata sheria za mikusanyiko kabla ya fainali ya mchezo wa NRL
  • ACT yarekodi kesi mpya 38 ndani ya jamii
  • Tasmania yarekodi kesi moja ndani ya jamii

Victoria

Victoria imerekodi kesi mpya 1,220 za COVID-19 ndani ya jamii pamoja na vifo vitatu.

Kiongozi wa jimbo hilo Daniel Andrews amesema vizuizi vinahusu kulinda mfumo wa afya nakuheshimu watalaam wa afya. “Kitakacho kuwa uhuru kwetu, kitakuwa ni wakati mgumu kwa mfumo wetu wa afya", alisema.

Jana polisi waliwakamata watu 109, katika maandamano dhidi ya chanjo mjini Melbourne.

Michelle Spence, ni meneja wa waaguzi wa kitengo cha hali mahtuti katika hospitali ya Royal Melbourne amesema tangu Julai, Victoria imekuwa na watu 90 ndani ya kitengo cha hali mahtuti na, hakuna hata mtu mmoja humo aliye kuwa ame pata chanjo kamili.

Pata kituo cha chanjo karibu yako.

New South Wales

NSW imerekodi kesi mpya 667 za COVID-19 ndani ya jamii, pamoja na vifo 10, wakati eneo la Greater Sydney lime maliza siku 100 ndani ya amri ya makatazo yakutoka nje.

Waziri wa Afya Brad Hazzard amewahamasisha wakaaji, wafanye tahadhari masaa machache kabla ya fainali ya mchezo wa NRL. "Nyumba yako inaendelea kuwa moja ya sehemu za hatari sana kwa upande wa usambaaji wa virusi," alisema.

Kuanzia Oktoba 11, mtu yeyote jimboni NSW ambaye ni mtu wa karibu wa mtu ambaye amepatwa na COVID-19 na amepata chanjo kamili, ata takiwa kufanya vipimo nakujitenga kwa siku saba badala ya siku 14.

Bonyeza hapa kuomba miadi ya chanjo yako leo. 

Hali ilivyokuwa nchini Australia katika masaa 24 yaliyo pita
  • ACT imerekodi kesi mpya 38 ndani ya jamii, watu 16 kati yao wakiwa ndani ya jamii wakati walikuwa katika hali ambukizi.
  • Jimboni Tasmania mvulana mmoja amepatwa na COVID-19, baada yakutua mjini Launceston kutoka Melbourne.
  • Queensland haija ripoti kesi yoyote mpya. Fainali ya mchezo wa NRL kati ya Penrith Panthers na South Sydney Rabbitohs, ita endelea jioni ya leo katika kitongoji cha Lang Park.
  • Jimbo la Kusini Australia liliripoti kesi mpya mbili mchana wa jana.
Stay home Safe Life - SBS Radio
Stay home Safe Life - SBS Radio Source: SBS Radio

Karantini, safari, zahanati za vipimo na malipo ya janga

Karantini na masharti yavipimo husimamiwa nakutekelezwa na serikali zamajimbo na wilaya:

NSW Safari & usafiri na Karantini

VIC Vibali vya safariWasafiri wa ng'ambo na Karantini

ACT Usafiri na Karantini

NT Safari na Karantini

QLD Safari na Karantini

SA Safari na Karantini

TAS Safari na Karantini

WA Safari na Karantini

Kama unataka safiri ng'ambo, unaweza omba kibali mtandaoni. Bonyeza hapa kwa taarifa zaidi kuhusu masharti yakuondoka Australia. Kuna hatua za mpito kwa safari zakimataifa ambazo hutathminiwa mara kwa mara na serikali, nakuchapishwa kwenye tovuti ya Smart Traveller.



Tazama rasilmali zilizo tafsiriwa za huduma yamawasiliano ya shirika la afya ya tamaduni nyingi ya NSW:

COVID-19 Vaccination Glossary
Appointment Reminder Tool.


Zahanati za vipimo katika kila jimbo na wilaya:

NSW 

Victoria 

Queensland 

South Australia 

ACT 

Western Australia 

Tasmania

Northern Territory 


Taarifa kuhusu malipo ya janga katika kila jimbo la wilaya:

NSW 

Victoria 

Queensland 

South Australia 

ACT 

Western Australia 

Tasmania
Northern Territory


Share

3 min read

Published

By SBS/ALC Content

Presented by Gode Migerano

Source: SBS




Share this with family and friends


Follow SBS Swahili

Download our apps

Listen to our podcasts

Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service

Watch now