Taarifa mpya kuhusu COVID-19: Victoria kuondoa vizuizi mapema, mpangilio wa usafiri kati ya Australia na NZ kuanza tena

Hii ni taarifa mpya kuhusu Coronavirus nchini Australia kwa 17 Oktoba 2021.

Brighton, St Kilda, Victoria

Brighton, St Kilda, Victoria Source: AAP/DANIEL POCKETT

  • Victoria yaondoa vizuizi mapema kuliko ilivyo tarajiwa
  • NSW yafikia 80% ya watu ambao wamepata chanjo mbili
  • Mpangilio wa usafiri kati ya Australia na New Zealand kuanza tena wiki hii
  • Serikali ya Australia yanunua 'Tiba' ya COVID-19

Victoria

Victoria yarekodi kesi mpya 1,838 za COVID-19 ndani ya jamii pamoja na vifo saba.

Kuna watu 777 ambao kwa sasa wako hospitalini, 151 wako katika kitengo cha huduma mahtuti pamoja na watu 94 ambao wanapumua kwa msaada wa mashine.

Kiongozi wa jimbo hilo Daniel Andrews alitangaza uamuzi wakuondoa vizuizi mapema kuliko ilivyo tarajiwa. Vizuizi vitaregezwa kuanzia usiku wa manane wa Alhamisi 21 Oktoba. “Vizuizi vikiondolewa, hapatakuwa vizuizi kwa watu kuondoka nyumbani, hapatakuwa amri yakubaki ndani," Kiongozi huyo alisema.

Asilimia 89 yawatu wa Victoria wenye umri wa miaka 16 na zaidi, wame pata dozi moja ya chanjo ya COVID, na asilimiia 65.5 yawatu wa Victoria wamepata chanjo kamili.

Pata kituo cha chanjo karibu yako.

New South Wales

NSW imerekodi kesi mpya 301 za COVID-19 ndani ya jamii, pamoja na vifo 10.

Kiongozi wa jimbo hilo Dominic Perrottet alisema jana kuwa NSW imefikisha lengo la 80% la chanjo mbili, hali ambayo inamaanisha kuwa kuanzia kesho vizuizi vya ziada vita ondolewa.

Bw Perrottet ametangaza uwekezaji wa $130 milioni kwa afya ya akili.

"Sisi ni jimbo la kwanza Australia kuanza kutoa mafunzo kwa watu 275,000 kwa swala la kuzuia kujiua na huduma ya kwanza ya afya ya akili," Waziri wa Afya ya Akili Bronnie Taylor alisema.

Bonyeza hapa kuomba miadi yako ya chanjo leo. 

Hali ilivyokuwa nchini Australia katika masaa 24 yaliyo pita
  • Serikali ya shirikisho imenunua tiba elfu kumi na tano za Ronapreve.
  • Usafiri bila karantini utaanza tena kati ya NSW na Vic na sehemu za NZ kuanzia usiku wa manane wa Jumanne 19 Oktoba.
  • ACT imeripoti kesi mpya 33 za maambukizi ya COVID.
  • Tasmania haija rekodi kesi yoyote mpya.
  • Serikali ya Queensland haija weka tarehe yakufungua tena mipaka yake.

Karantini, safari, zahanati za vipimo na malipo ya janga

Karantini na masharti yavipimo husimamiwa nakutekelezwa na serikali zamajimbo na wilaya:

NSW Safari & usafiri na Karantini

VIC Vibali vya safariWasafiri wa ng'ambo na Karantini

ACT Usafiri na Karantini

NT Safari na Karantini

QLD Safari na Karantini

SA Safari na Karantini

TAS Safari na Karantini

WA Safari na Karantini

Kama unataka safiri ng'ambo, unaweza omba kibali mtandaoni. Bonyeza hapa kwa taarifa zaidi kuhusu masharti yakuondoka Australia. Kuna hatua za mpito kwa safari zakimataifa ambazo hutathminiwa mara kwa mara na serikali, nakuchapishwa kwenye tovuti ya Smart Traveller.



Tazama rasilmali zilizo tafsiriwa za huduma yamawasiliano ya shirika la afya ya tamaduni nyingi ya NSW:

COVID-19 Vaccination Glossary
Appointment Reminder Tool.


Zahanati za vipimo katika kila jimbo na wilaya:

NSW 

Victoria 

Queensland 

South Australia 

ACT 

Western Australia 

Tasmania

Northern Territory 


Taarifa kuhusu malipo ya janga katika kila jimbo la wilaya:

NSW 

Victoria 

Queensland 

South Australia 

ACT 

Western Australia 

Tasmania
Northern Territory


Share

3 min read

Published

By SBS/ALC Content

Presented by Gode Migerano

Source: SBS




Share this with family and friends


Follow SBS Swahili

Download our apps

Listen to our podcasts

Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service

Watch now