Taarifa mpya ya UVIKO-19: WA yarekodi kesi mpya 12,390; Victoria yaripoti ongezeko ya watu wanao lazwa hospitalini

Hii ni taarifa yako mpya kuhusu UVIKO-19 nchini Australia kwa 10 Mei 2022.

People wearing face masks walk in the Melbourne CBD, Thursday, July 15, 2021. Victoria has reported two new locally acquired COVID-19 cases, on top of the 10 reported in Thursday's official figures. (AAP Image/Luis Ascui) NO ARCHIVING

The number of new COVID-19 surged in most Australian states and territories. Source: AAP Image/Luis Ascui

Jumanne, Australia iliripoti vifo 43 vya UVIKO-19 vilivyo jumuisha vifo 18 Victoria na vifo 17 New South Wales. 

Magharibi Australia imerekodi idadi ya juu zaidi ya kila siku ya kesi mpya za UVIKO-19 (12,390), tangu mwanzo wa janga. Iliripoti pia vifo sita vyakihistoria.

Idadi ya kesi mpya ziliongezeka kote nchini Australia, Victoria ikiripoti idadi kubwa zaidi ya maambukizi ya kila siku (12,722) na idadi ya watu walio lazwa hospitalini (519) tangu 4 Aprili. 

Tazama maendeleo mapya ya UVIKO-19 kwa kesi mpya, kulazwa hospitalini na vifo kote nchini Australia hapa

Utawala wa Bidhaa za Matibabu (TGA) inachunguza nakutathmini ripoti za myocarditis (kuvimba kwa moyo) na pericarditis (kuvimba kwa tishu inayo zunguka moyo) katika vikundi vya vijana kutoka chanjo za Pfizer na Moderna.

Imesemwa kuwa myocarditis inajulikana ila madhara ya baadae ambayo "ni nadra". Kawaida ni ya muda mfupi na watu wengi, hupata nafuu baada ya siku chache. Ni kawaida zaidi miongoni mwa wavulana wenye miaka kati ya 12-17 baada ya dozi ya pili.

Kundi la ushauri lakiufundi la Australia kwa chanjo, lina zingatia dozi ya nne (ya majira ya baridi) kwa vikundi vya ziada.

Kwa sasa, dozi ya nne imependekezwa kwa watu wazima wenye miaka 65 na zaidi, wakaazi ndani ya makazi ya huduma ya wazee na walemavu, watu wenye miaka 16 na zaidi ambao wana matatizo sugu ya kinga ya mwili, na watu kutoka jamii yawa Australia wa asili na Torres Strait Islanders wenye miaka 50 na zaidi.

 

 


Soma kuhusu Chanjo za UVIKO-19 katika Kiswahili


Pata zahanati ya kupimia UVIKO-19

ACT   New South Wales   Northern Territory   Queensland   

South Australia   Tasmania   Victoria   Western Australia  

Sajili matokeo ya kipimo chako cha RAT hapa, kama ni chanya 

ACT   New South Wales   Northern Territory   Queensland    

South Australia   Tasmania   Victoria    Western Australia


Jua kuhusu unachoweza na kile ambacho hauwezi fanya popote nchini Australia

Kabla uende ng'ambo, tazama masharti mapya ya usafiri na ushauri

Kama unahitaji msaada wa fedha, tazama chaguzi zako ni gani

Hapa kuna msaada waku saidia kuelewa maneno yakiufundi ya UVIKO-19 katika Kiswahili


Soma taarifa zote kuhusu UVIKO-19 katika Kiswahili kwenye tovuti ya SBS kuhusu Coronavirus.  


Share

2 min read

Published

Presented by Gode Migerano




Share this with family and friends


Follow SBS Swahili

Download our apps

Listen to our podcasts

Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service

Watch now