Wafanyakazi wa uokoaji waliwaokoa waathirika zaidi kutoka kwenye miti na mapaa ya nyumba siku ya Alhamisi, wiki moja baada ya kimbunga kuteremka kupitia kusini mwa Afrika na kusababisha mafuriko mabaya ambayo yameua mamia ya watu na maelfu kupoteza makazi yao.
Helikopta zilizunguka juu ya maji ya mafuriko yenye rangi nyekundu-kahawia hivi, ndege hizo zilikuwa zikitafuta watu kuwavukisha hadi jiji la Beira, ambalo ni makao makuu ya operesheni kubwa ya uokoaji nchini Msumbiji.
Idadi ya vifo kwa sasa ni 242, Waziri wa Ardhi na Mazingira Celso Correia alisema, akiongezea kuwa idadi ya waliofariki iliongezeka wakati wafanyakazi wa uokoaji walipokuwa wakipata miili iliyofichwa na maji ya mafuriko ya sasa.
Correia alizungumza katika mkutano wa wanahabari mapema kuwa karibu watu 15,000, wengi wao wagonjwa sana, bado wanahitaji kuokolewa. "Vita yetu kubwa ni dhidi ya muda," alisema, na kuongeza kuwa watu 3,000 wameokolewa hadi sasa.
Katika nchi ya jirani ya Zimbabwe, idadi ya vifo vilisababishwa na kimbunga Idai, iliongezeka hadi kufikia 139. Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya chakula (WFP), ambalo ndilo linaloshughulikia ugawaji wa chakula walisema, watu 200,000 wa Zimbabwe wanahitaji msaada wa chakula kwa muda wa miezi mitatu.
Nchini Malawi, watu 56 walithibitishwa kufariki.
Share

