Fainali hiyo iliwaniwa na Macarthur FC ya daraja la kwanza la ligi kuu ya Australia, dhidi ya Sydney United 58 FC ya daraja la pili la Australia.

Kama ilivyo tarajiwa Macarthur FC ilitawala fainali hiyo kwa muda mrefu, na katika dakika ya 32 Al Hassan Toure alifunga goli la kwanza kupitia penati baada ya mshambuliaji wao Daniel Arzani kutegwa ndani ya sehemu ya hatari ya Sydney United 58 FC.

Sydney United 58 FC ilianza kipindi cha pili kwa kasi, ikitafuta goli lakusawazisha hata hivyo juhudi zao hazikuvuna matunda yoyote na waliadhibiwa tena kupitia penati katika dakika ya 90 nahodha wa Macarthur FC alipo funga goli la pili nala ushindi. Muda mfupi baadae mwamuzi wa mechi alipuliza kipyenga cha mwisho, na Macarthur FC wakaanza sherehe za ushindi wao wamagoli 2 kwa sufuri.

Kupitia ushindi huo mwalimu wa Macarthur FC nyota wa zamani wa Manchester United na Trinidad & Tobago, Dwight Yorke ameingia katika historia kama mwalimu wa kwanza aliye ipa Macarthur FC kombe la kwanza.

