Watu hamsini na moja, wamefariki dunia baada ya basi walilokuwa wanasafiria kupinduka na paa lake kuharibika vibaya katika ajali iliyotokea magharibi mwa Kenya mapema asubuhi ya Jumatano, polisi walisema.
"Kwa bahati mbaya tumewapoteza watu 51," Mkuu wa Polisi Kenya Joseph Boinnet aliiambia redio ya Capital FM.
Kwa mwajibu wa polisi, basi hilo lilikuwa likisafiri kutoka Nairobi kuelekea mji wa magharibi wa Kakamega ikiwa imebeba abiria 52.
Shirika la msalaba mwekundu la Kenya liliandika kwenye mtandao wa Twitter kuwa, basi lilipinduka. Ingawaje, taarifa zaidi ya chanzo cha ajali hiyo hazikufahamika haraka.
Video kutoka eneo la ajali zinaonyesha basi chakavu jekundu likiwa limelala ubavu, viti na baadhi ya mabaki ya vyuma vikionekana wazi baada ya paa la basi hilo kuezuliwa na kutupiliwa mbali kutoka basi hilo.
Watu kadhaa walionekana kuzagaa eneo la ajali huku baadhi ya vitu vikionekana kusambaa eneo kubwa.
Takwimu rasmi zinaonyesha kuwa takribani watu 3,000 huwa kwa ajali za gari kila mwaka nchini Kenya, lakini shirika la afya duniani linakadiria idadi hiyo kuwa kubwa hadi watu 12,000.
Mnamo mwezi Desemba 2017, watu 36 walikufa kwa ajali ya gari baada ya basi na roli kukoganga uso kwa uso.
Mwaka 2016 zaidi ya watu 40 walifariki dunia wakati gari la mafuta lilipokosa mwelekeo na kuyagonga magari mengine na kulipuka katika barabara kuu.
Share

