Kiongozi wa tume huru ya uchaguzi ya DRC (CENI) Corneille Nangaa, alieleza taaifa na waandishi wa habari kuwa, tume hiyo haikuwa tayari kufanya uchaguzi huo baada ya mashine za uchaguzi kuteketea katika moto ulio choma jengo ambalo vilikuwa viki hifadhiwa ndani.
Bw Nangaa aliongezea kuwa "Uchaguzi wa urais, bunge pamoja na uchaguzi wa mikoa utafanywa tarehe 30 Disemba, 2018,"
Kwa mujibu wa taarifa kutoka CENI, wiki jana asilimia 80 ya mashine za kura ziliteketezwa kwa moto ndani ya jengo moja mjini Kinshasa. Tukio hilo lime athiri uwezo wa CENi kuhakikisha kura zitapigwa nchini kote siku ya uchaguzi, ndipo tume hiyo ika amua kuahirisha uchaguzi mkuu hadi tarehe 30 Disemba.
SBS Swahili ina andaa mjadala maalam kuhusu uchaguzi wa urais wa DR Congo, mjadala huo uta anza saa tisa mchana kwa masaa ya mashariki ya Australia, Jumapili 23 Disemba 2018.
Share

