
This article is more than 4 years old
Breaking
Dr William Ruto atangazwa Rais mteule wa Kenya
Baada ya vurugu iliyotishia kufutwa kwa tangazo la mshindi wa uchaguzi wa rais, hatimae Kenya imempata rais wa tano.
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya Kenya, Wafula Chebukati ametangaza rasmi kuwa Dr William Ruto ndiye mshindi wa uchaguzi wa urais wa 2022.
Tangazo hilo limejiri licha ya makamishna wanne wa tume hiyo, kujiweka mbali na tangazo hilo pamoja na mwenyekiti Chebukati kusema kuwa baadhi ya wafanyakazi wake walikuwa wame kamatwa na vyombo vya usalama bila sababu.
SBS Swahili itakuletea taarifa zaidi kuhusu tangazo hili hivi punde.
Share
