Kwa mujibu wa katiba ya Kenya, kiapo cha urais lazima kichukuliwe kati ya saa nne asubuhi na saa nane mchana. Sherehe hiyo ilisimamiwa na Martha Koome, Jaji Mkuu wa Mahakama ya Upeo ya Kenya.
Uwanja wa Kasarani ulijaa muda mfupi baada yakufunguliwa mida ya saa kumi unusu ya asubuhi. Marais wa nchi kadhaa walijumuika katika sherehe hiyo, na Rais Kenyatta alitimiza ahadi yake yakukabidhi mamlaka kwa amani licha yakumpigia debe mpinzani wa Dr Ruto katika kampeni za uchaguzi mkuu. Kabla yakumkabidhi Dr Ruto mamlaka, Rais Kenyatta alikagua gwaride kwa mara ya mwisho.
Rais Dr Ruto ameingia katika historia ya siasa za Kenya, kuwa mtu aliyeshinda chaguzi zote alizo wania kwa mara ya kwanza.