Vikosi vya usalama vya Misri, vimewaua wanaoshukiwa kuwa wapiganaji 20 hivi karibuni kaskazini mwa Sinai Peninsula mpakani mwa Libya.
Jeshi la nchi hiyo limesema kuwa, vikosi vyake viliharibu maficho 18 na vituo vya silaha,
huku wakitegua mabomu 41 na kuwakamata watuhumiwa83.
Jeshi limesema, mashambulizi ya anga, yaliharibu zaidi ya magari 39 magharibi mwa jangwa, ambapo magari hayo yalikuwa yamebeba silaha na mabomu.

An air strike has reportedly killed several Egyptian militants in Sinai. Source: AAP
Misri, kuanzia mwezi wa pili, walizindua operesheni ya kitaifa kupambana na waasi hao wapiganaji.
Imejitahidi kupambana na uasi wa muda mrefu huko Sinai ambayo sasa inahusishwa na kikundi cha Kiislamu cha IS.
Share

