Wanaharakati na mashirika ambayo hutoa huduma kwa wahanga na waathiriwa wa visa vya unyanyasaji wa nyumbani, wamesisitiza kuwa janga la COVID-19 limeongeza hatari ya swala hili haswa kama watu hawatambui dalili na ishara za visa vya unyanyasaji wa nyumbani.
Rosemary Kariuki ni mwanaharakati wa jamii, alikuwa mzungumzaji kwenye uzinduzi waripoti maalum kuhusu unyanyasaji wa nyumbani, ambayo iliandaliwa kwa ushirikiano kati ya Chuo cha Western Sydney na shirika la Great Lakes Agency for Peace International (GLAPD). Alipozungumzia swala hili alifafanua nakuweka wazi dalili na ishara za unyanyasaji wa nyumbani akitomfano kuwa ni: "saa zote ukiongea nasima anataka jua unaongea na nani, ukitaka enda omba kanisani au katika msikiti unao penda, anataka tu uende kwa yake, hataki utembelee wala utembelewe na marafiki, ukipika chakula ambacho hapendi hiyo ni kelele". Image
Wanawake wengi na baadhi ya wanaume, wamejipata katika hali kama hizo zilizo elezewa na Bi Rosemary. Wengi wao wakisalia namakovu yakisaikolojia ambayo huwa yana chukua muda mrefu sana kupona.
Bi Eve ni mfanyakazi wa jamii katika shirka la Great Lakes Agency for Peace International (GLAPD), alipozungumzia hoja hii aliwahamasisha wanawake kwa wanaume wanao kabiliwa kwa matatizo ya unyanyasaji wa nyumbani kuwa; "usiteseke mwenyewe, haijalishi unakotoka njoo kwetu tutakupa usaidizi, ukitueleza unachopitia tutakusaidia aau kukutuma sehemu unaweza saidiwa zaidi. Kama mama anapitia matatizo hayo, yatawafikia watoto pia na hatutaki wapitie haya maneno".