Les alikuwa mmoja wa wana harakati wa kwanza, walio kuza soka nchini Australia akishirikiana na rafiki yake wa karibu na mchezaji wa zamani wa taifa Johnny Warren.

Les Murray na Johnny Warren wazindua kitabu chao "Mr & Mrs Soccer" Source: Getty Images AsiaPac
Licha ya rafiki yake kuaga dunia kabla ya Australia kurejea katika michuano ya kombe la dunia, baada ya miaka mingi ya ukame Les Murray aliongoza matangazo hayo yaliyo peperushwa ndani ya nyumba zama milioni za wapenzi wa soka nchini Australia kila siku.

Mtangazaji wa soka mstaafu wa SBS Australia, Les Murray Source: The World Game
Hakuna shindano kubwa la soka ambalo Les hakushiriki, na aliwaongoza watangazaji wa SBS kwa mara ya mwisho katika moja ya nchi aliyo penda zaidi katika kombe la dunia la 2016 nchini Brazil. Les aliwaaga watazamaji kwa mara ya mwisho akizungukwa na marafiki na watangazaji wenza, naku acha historia na urithi ambao watangazaji wengi wana iga hadi sasa.

Mtangazaji wa soka wa SBS Australia, Les Murray akiaga watazamaji kwa mara ya mwisho Source: The World Game
Hata kama jamii ya kandanda ya Australia imempoteza mmoja wa watoto wake mpendwa, urithi wake utaishi milele.
Share

