Maelfu yamashabiki wa FC Barcelona, walijumuika katika uwanja wa Accor mjini Sydney kutimiza ndoto zao zakutazama mechi ya timu yao pendwa.
Wengi wao ilikuwa mara ya kwanza kufika uwanjani kutazama timu yao ikicheza, wakati wengine wenye uwezo zaidi zaidi kiuchumi ilikuwa fursa yao kushabikia timu yao nchini mwao.
Mashabiki wengi wali eleza Idhaa ya Kiswahili ya SBS, matumaini na matarajio ya mechi hiyo pamoja nakutabiri matokeo ya mechi hiyo wengi wao wakitarajia timu ya A-League All Stars kurudi nyumbani na makapu yamagoli.
Hata hivyo, wachezaji wa A-League All Stars walionesha vipaji vyao na, waliunda nafasi nzuri zaidi kuliko FC Barcelona zakushinda mechi hiyo lakini ubora wa wapinzani wao uliwanyima ushindi na hatimae walipoteza mechi hiyo magoli tatu kwa mbili. Mashabiki walishuhudia pia makabiliano yakihistoria, kati ya wachezaji wawili wajina Adama Traore kutoka FC Barcelona na A-League All Stars.

Mashabiki wa FC Barcelona ndani ya uwanja wakisubiri mwanzo wa mechi dhidi ya A-League All Stars. Source: SBS Swahili

Mashabiki wa FC Barcelona baada yakuzungumza na SBS Swahili, nje ya uwanja wa Accor mjini Sydney, Australia. Source: SBS Swahili

Adama Traore wa FC Barcelona, akabwa na Adama Traore wa A-League All Stars, katika mechi yakirafiki mjini Sydney, Australia Source: AAP