Wataalmu wa afya wanasema, mlipuko huo hatari wa Ebola ulianzia vijijini nchini humo, umetawanyika hadi mjini hivyo kuzua hofu kubwa katika ukanda huo.
Mlipuko mpya umetangazwa rasmi tarehe 8 Mei ikiwa vimefikia vifo 23 hadi sasa, lakini mwanzo mlipuko huo ulitangazwa kutokea vijijini sehemu ya jimbo la Equateur, Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo.
Lakini wizara ya afya nchini humo na Shirika la Afya Duniani (WHO) siku ya Alhamis walisema, wamethibitisha mlipuko wa gonjwa hilo kuwepo Mbandaka, ambao ni mji mkuu wa Equateur kama kilomita 150 (90 miles) kutoka eneo la Bikoro ambapo mlipuko ulipoanzia.

People suspecting of Ebola Virus wait at a treatment centre in Bikoro Democratic Republic of Congo. Source: AAP
Madaktari wa kujitolea wajulikanao kama ’Doctors Without Borders (MSF)’, waliwanukuu maafisa wa eneo hilo wakisema, takribani watu 514 wanaaminika kukutana na wagonjwa wa Ebola na kwa sasa wako chini ya uangalizi.
Peter Salama, msimamizi wa masuala ya dharura kutoka WHO, amesema kuenea kwa ugonjwa huo mjini, kunayanya iwe ngumu kupambana nao, kitu kitakachotegemea kutambua na kutenga wanaoshukiwa kupata maradhi.
Idadi ya watu katika mji wa Mbandaka kwa mujibu ya makadirio yaliyopita ni watu takribani 700,000 hadi milioni 1.2.
Katika msimu uliopita, milipuko mingi ya Ebola nchini DRC, ilikuwa ikitokea vijijini na ilikuwa rahisi kupambana nao lakini kwa sasa tuna zaidi ya milioni moja wako kwenye hatari ya gonjwa," alisema Salama mjini Geneva.
WHO wametangaza kutuma wataalamu 30 kwenye mji wa Mbandaka, wkaati MSF nao walisema, watatuma tani kadhaa za madawa kama sehemu ya msaada kuoambana na janga hilo.
Share

