Nyota huyo wa zamani wa Ligi ya Uingereza, alipata bao baada ya dakika 21 kabla ya kutoa asisti dakika saba kabla ya mechi kumalizika ambapo Xu Xin aliongeza bao la pili la Taishan.
Matokeo hayo yalinyanyua uongozi wa Shandong Taishan kileleni mwa ligi ya CSL ambapo kwa sasa ina alama 51 ambazo haziwezi kufikiwa na timu zingine.
Akiwa amevalia kitambaa cha unahodha, Fellaini aliiweka Shandong mbele wakati kipa wa Hebei, Bao Yaxiong aliposhindwa kufanya vya kutosha kuzuia mpira uliokatwa wa Jin Jingdao kutoka upande wa kulia, na kumwacha kiungo huyo wa zamani wa Ubelgiji kuruka juu ya mstari.

Marouane Fellaini wakati akiwa na Manchester United Klabu Bingwa Ulaya Source: Getty Images

Fellaini akiwa katika majukumu uwanjani ligi ya Uchina Source: Getty Images
Dakika saba kabla ya mchezo kumalizika, Fellaini alihusika tena, safari hii akimuona Bao akiokoa mpira wa kichwa pekee kwa Xu kufunga kwenye mpira uliorudi na kuifungia Shandong.
Ubingwa wa Shandong kunaashiria mwisho wa enzi iliyotawaliwa na vilabu vinavyoungwa mkono kwa kiasi kikubwa na wafanyabiasha wa majumba wa Uchina wenye matumizi makubwa.