Watu wanne wanaaminika kufariki dunia na mtuhumiwa kukamatwa baada ya shambulio la risasi huko Darwin.
Tukio hilo lilianza kwa taarifa kuwa mtu mmoja alionekana akipiga risasi hovyo mida ya saa 11.50 jioni leo Jumanne.
Shambulio hilo la risasi limetokea kwenye kitongoji cha Woolner, na mtuhumiwa alielezewa kuwa ameshika bunduki na ni hatari.
Hakukamatwa kwa muda wa saa nzima hivi.
Polisi walithibitisha kumkamata mtu huyo mwenye umri wa miaka 45.
Mwanzo iliaminika mtu mmoja alikuwa ameua, polisi kwa sasa wanasema watu wanne wameua.
Siyo tukio la kigaidi
Kutoka Uingereza, Waziri mkuu Scott Morrison amesema "ushauri wetu ni kwamba hili siyo tukio la kigaidi".