Mlipuko wa roli la mafuta waua kadhaa Tanzania

Zaidi ya watu 60 wamekufa na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya tanki la mafuta ambalo lilianguka nchini Tanzania kulipuka wakati watu walikuwa wakijaribu kuchota mafuta.

Fire fighters try to put off fire of the patrol tanker, in Tanzania

Fire fighters try to put off fire of the patrol tanker, in Tanzania. Source: AP

Lori lililokuwa limeharibika lilipuka mashariki mwa Tanzania wakati watu waliokuwa wakijaribu kuchukua mafuta hayo, na kuua watu wasiopungua 62 katika moja ya matukio mabaya zaidi ya aina yake katika nchi ya Afrika mashariki.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Tanzania TBC, lilionyesha takwimu za polisi, wakisema watu wasiopungua 70 wamejeruhiwa wakati wa mlipuko katika mji wa Morogoro, karibu km200 kutoka kwa kitovu cha uchumi cha Dar es salaam.

Mkuu wa Mkoa, Steven Kebwe aliiambia runinga ya Azam kuwa wengi walipata majeraha ya moto.

Mashahidi walisema umati wa watu ulikuwa umekusanyika karibu na tanki la mafuta baada ya kutokea ajali mapema Jumamosi, na watu wengine walikuwa wakijaribu kuchota mafuta wakati lori lilipolipuka moto.

Video iliyosambaa katika mitandao ya kijamii inaonyesha watu wakikusanya mafuta kuweka kwenye vidumu kabla ya mlipuko.

Katika taarifa ya rambirambi, Rais wa Tanzania John Magufuli alisema alifadhaika watu walishambulia magari yaliyohusika na ajali badala ya kutoa msaada.

Wakazi huuliwa mara kwa mara na milipuko wakati wanaiba mafuta kutoka kwenye maroli yanayoharibika huko mashariki mwa Afrika. Wale ambao wanaiba mafuta kawaida hutarajia kuweza kuuza kwa bei rahisi kwa madereva.


Share

Published

By Frank Mtao

Share this with family and friends


Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service