Wanaspoti kutoka nchi washiriki duniani kote, walijumuika ndani ya uwanja wa Olimpiki mjini Tokyo, katika hafla ya uzinduzi wa michezo hiyo.

Wapeperushaji wa bendera ya Australia Cate Campbell na Patty Mills waongoza wachezaji wa Australia katika sherehe ya uzinduzi ya michezo ya Olimpiki, Tokyo 2020 Source: Visual China Group via Getty
Tofauti na uzinduzi wa michezo ya Olimpiki ya kabla ambako maelfu yamashabiki walijaa ndani ya uwanja wa michezo na hata nje ya uwanja kushuhudia uzinduzi huo, uzinduzi wa Tokyo 2020 ulifanyika bila mashabiki kwa sababu ya hofu ya usambaaji wa virusi vya COVID-19.
Watu wengi walikuwa na hofu kuwa michezo hiyo ita ahirishwa au kufutwa tena, baada ya ongezeko ya visa vya maambukizi ya COVID-19 nchini Japan, pamoja na katika nchi ambako baadhi ya wachezaji husika wanatoka.

Thomas Deng nahodha wa timu ya mpira wa miguu ya Olimpiki ya Australia, Source: Getty Images
Wanachama wa jamii ya Afrika Mashariki waliwakilishwa kwa fahari na kijana wao, Thomas Deng aliye zaliwa mjini Nairobi, Kenya ambako familia yake walikuwa wakimbizi kutoka Sudan Kusini.
Thomas na familia yake waliwasili nchini Australia, akiwa na miaka sita na sasa ndiye nahodha wa timu ya taifa ya mpira wa miguu ya olimpiki. Thomas aliongoza timu yake kupata ushindi, dhidi ya wababe wa soka duniani Argentina katika mechi ya kwanza ya kundi lao mjini Tokyo, Japan.