Wengi wao wamekabiliana na maswali na maamuzi magumu, kuhusu hatma ya biashara zao wakati ambapo mamlaka katika kila jimbo na mkoa nchini wana endelea kuregeza nakukaza vizuizi vyakudhibiti usambaaji wa maambukizi ya virusi vya UVIKO-19.
Katika jimbo la Kusini Australia, mjasiriamali Martin ali eleza idhaa ya Kiswahili ya SBS Kwamba "alikuwa amefika mwisho wa uvumilivu kiasi kwamba aliamua kuacha biashara yake nakutafuta kazi katika sekta nyingine kwa ajili yakumudu gharama za familia yake". Ila baada ya mamlaka husika kuregeza vizuizi kwa mikusanyiko namatukio katika jamii, Bw Martin amefufua biashara yake tena yaku tengeza filamu nakupiga picha za harusi na katika matukio mengine.

Young Martin akiwa kazini Source: Young Martin
Nako Jimboni Victoria, Bw Tony ambaye biashara yake yakuwasaidia watu kufanya mazoezi baada yakupata jeraha au kwa wanao taka boresha afya yao imijipata katika njia panda. Serikali ya jimbo hilo imetoa ruhusa kwa biashara ndogo kuanza kuwahudumia wateja tena, ila ni wateja walio pata chanjo tu ndiwo wanao ruhusiwa kuhudumiwa. Licha yakupewa idhini yakufungua milango ya biashara yake tena, Bw Tony amesalia na maamuzi magumu kwa jinsi yakuwaeleza baadhi yawateja wake kuwa "hawawezi pokea huduma kwa sababu ya hali yao ya chanjo".
Image
Na jimboni New South Wales, hali imekuwa chanya kwa Mdm Youvip. Biashara yake yakutengeza video nakupiga picha za matukio ilikuwa inaelekea pabaya kabla kiongozi wa jimbo hilo, atangaze ruhusa ya biashara kama zake kuanza kazi tena. Mdm Youvip, alifunguka kuhusu masaibu aliyo kabiliana nayo kama mjasiriamali wakati wa vizuizi vya UVIKO-19.

Mdm Youvip akiwa kazini Source: Mdm Youvip