Helikopta ya kijeshi ilipata ajali eneo la mkoa wa Oromiya nchini Ethiopia, na kuua watu wote 18, ikiwa ni pamoja na askari 15, taarifa ya shirika la habari la serikali la Fana lilitaarifu.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Fana, watu hao wengine watatu waliofariki katika ajali hiyo, walikuwa ni raia.
Waziri wa baraza la mawaziri wa mkoa wa Oromiya, Addisu Arega alithibitisha ripoti ya Fana na akaandika hivi: "Abiria wote walifariki dunia, sababu ya ajali hiyo bado inafanyiwa uchunguzi. Tunawapa pole wafiwa wote."
Helikopta ilikuwa ikisafiri kutoka mji wa Mashariki wa Ethiopia wa Dire Dawa na kuelekea Bishoftu karibu na kilomita 60 kusini mwa mji mkuu Addis Ababa, alinukuliwa akisema waziri huyo Bwana Addisu.
Share

