Wanasiasa wakitaifa watano naibu waziri mkuu wa zamani Barnaby Joyce akijumuishwa, wamefurushwa ofisini baada ya mahakama kuu kutoa uamuzi wake kwa kesi ya wanasiasa walio kuwa wame kumbwa kwa utata wa uraia pacha.
Naibu Waziri Mkuu Barnaby Joyce, Seneta Fiona Nash, maseneta wa zamani wa chama cha Greens Scott Ludlam na Larissa Waters na Seneta wa chama cha One Nation Malcolm Roberts walipatwa kuwa ni raia wa nchi zingine, wakati waku wasilisha ombi lakuwania uchaguzi mkuu wa taifa wa 2016.
Seneta wa chama cha Nationals Matthew Canavan, aliye jiondoa katika baraza lamawaziri, na Seneta huru Nick Xenophon hawaku athiriwa kwa uamuzi wa mahakama kuu. Seneta Canavan ata endelea na majukumu yake kama Waziri wa Rasililimali na ukanda wa Kaskazini ya Australia.
Nafasi hizo tupu katika seneti sasa, zita amuliwa kupitia hesabu maalum ya kura zilizo pigwa katika uchaguzi wa 2016.
Wakati huo huo hatma ya Bw Joyce ita amuliwa kupitia uchaguzi mpya katika eneo bunge la New England tarehe 2 Disemba.
Share

