Viongozi mbalimbali wa kisiasa, wametoa salamu zao za rambirambi kufuatia kifo cha Waziri Mkuu wa zamani Bob Hawke, aliyefariki akiwa na umri wa miaka 89.
Waziri huyo wa Labor aliyedumu uongozini kwa miaka mingi, aliiongoza Australia kutoka 1983 hadi 1991, alifariki nyumbani kwake mjini Sydney siku ya Alhamisi.

Former prime minister Bob Hawke. Source: AAP
Katika maelezo yake, mkewe Blanche d'Alpuget alesema "Leo tumempoteza Bob Hawke, Muastralia muhimu - wengi wangesema, Muastralia muhimu wa zama za vita vilivyopita".