Wengi walio jaribu kutumia usafiri wa maji kuelekea maeneo ya Bukavu, walijipata wakitafuta mbinu mbadala za usafiri baada ya mamlaka kupiga marufuku usafiri kwa maji.
Alipo zungumzia swala hili, mkuu wa kamati ya dharura katika jimbo la Kivu kaskazini Muhindo Zangi, aliwashauri wakaaji wa Goma,"Nawaambia mandugu nama dada, mutoke mjini. Njia ya Ruchuru ikowazi nawahamasisha muitumie kuenda Butembo, Beni, Kanyabayonga, kule chakula inaweza patikana haraka. Wengine wenye wame enda Sake, nivuri. Mutoke muende Sake, muende huko mpandie Masisi kwa sababu hatutaki chukua hatari kubwa."
Imekaridiwa kufikia sasa mlipuko wa Volcano wa wiki jana umesababisha vifo takriban 30, nama elfu yawatu kutawanyika kila sehemu ya jimbo hilo. Idhaa ya Kiswahili ya SBS itawapa taarifa mpya kuhusu swala hili, punde tutakapo zikopea.