Zaidi ya watu milioni tano wamepewa uraia wa Australia tangu 1949.
Hatua muhimu ya mwisho ni sherehe ya kuapishwa kuwa raia, ambako watu hula kiapo nakukubali haki na jukumu la kuwa raia wa Australia.
Makazi yakudumu

Ruby Fowdar ni wakala wa uhamiaji katika shirika la Australian Immigration Agency lenye makao yake mjini Brisbane.
Amesema kuwa, short la kuwa raia wa Australia ni kuhakikisha unafuzu kutoa ombi la kuwa raia.
"Sharti kwa wahamiaji ni kuwa, kwanza wanastahili kuwa wakazi wakudumu," Fowdar amesema.
“Hata kama uko nchini Australia chini ya viza tofauti, kama viza ya wanafunzi au viza ya kufanya kazi, viza hizo hazizingatiwi kama viza za kudumu.
“Kwa hiyo lazima uwe raia wa kudumu kwanza kabla ya kuwa raia.
“Utakapokuwa mkazi wa kudumu na umeishi Australia kwa muda wa miaka minne, na umekuwa mkazi wa kudumu kwa mwaka mmoja, utafuzu kuwa raia wa Australia.”
Omba visa ya kudumu na upate taarifa za ziada hapa.
Muda ambao ombi lako litachukua

Idara ya Mambo ya ndani, imependekeza kutuma ombi lako kupitia mtandao ili liweze shughulikiwa haraka.
Kwa mujibu wa Damien Kilner kutoka idara ya familia na miradi ya uraia, kwa wanaotoa ombi wengi, muda ambao maombi yao ya uraia huchukua hushughulikiwa ni miezi 14.
Mtihani wa uraia
Wanaoomba uraia lazima pia wapite mtihani wa uraia wa Australia, kuonesha ujuzi wao wa Australia na uelewa wa wajibu na majukumu kama raia.

“Inachunguza kama unajua Kiingereza kwa kiwango cha msingi" Damien Kilner amesema.
“Mtihani huo unaofanywa kupitia mfumo wa kompyuta, huchukua nusu saa kumaliza kwa ujumla.”
Mtihani huo wenye maswali 20 na majibu ambayo unaweza chagua lililo sahihi, yanaambatana na kijitabu kwa jina la ‘Australian Citizenship – Our Common Bond’ kitabu hicho, kina taarifa kuhusu Australia, haki, demokrasia, serikali na sheria.
“Watu wanatarajiwa kuchunguza rasilimali hizo, wanapojiandaa kufanya mtihani huo, na watakapo jihisi wako tayari wanaweza fanya mtihani huo.”
Watu wengi hupita mtihani huo kwa alama ya 75%. Katika mwaka wa 2014 hadi 2015, 98.6% ya waliofanya mtihani huo walipita.
Pata taarifa za ziada hapa kuhusu mtihani wa uraia.
Pendekezo la mageuzi kwa sheria za uraia

Hali huenda ikawa ngumu kwa raia watarajiwa, wakati idara ya mambo ya ndani imependekeza kupiga marufuku kwa muda mfupi wanaotoa ombi la uraia kufanya mitihani baada ya kufeli mara kadhaa.
“Serikali imedokeza baadhi ya mageuzi," Kilner amesema. “Moja ya mageuzi ambayo yamedokezwa ni mara tatu, na ukifeli utatarajiwa kusubiri miaka miwili kabla urejee kufanya mtihani tena.”
“Ila mageuzi hayo yanategemea sheria hiyo kupitishwa bungeni."
Serikali imependekeza wanaotaka uraia wafanye mtihani tofauti wa Kiingereza, kuthibitisha wana kiwango sahihi cha kusoma, kuandika, kusikiliza na kuzungumza, mtihani huo ni sawa na kiwango cha 5.0 cha IELTS.
Watu wenye umri zaidi ya 60, watoto wenye umri chini ya 16, wenye matatizo yakusikia, kuzungumza au kuona na watu wenye uwezo mdogo wa afya ya akili na kimwili si lazima wafanye mtihani huo.

Mageuzi mengine makubwa ambayo yanaweza anza Julai, ni kuongezwa kwa muda ambao wakazi wakudumu wana stahili subiri kuwasilisha ombi la uraia kutoka mwaka mmoja hadi miaka minne, iwapo muswada huo utapitishwa bungeni.
Kiapo cha Uraia

Ombi la uraia litakapokubaliwa, walio wasilisha ombi lazima wahudhurie sherehe ya uraia kula kiapo cha uraia.
Kuna aina mbili za viapo, cha kwanza kinamtaja Mungu, na cha pili hakitaji Mungu.
“Kula kiapo ni hatua ya mwisho rasmi ya kuwa raia wa Australia” Damien Kilner wa idara ya mambo ya ndani amesema.
“Kwa watu wengi, wanatarajiwa kushiriki katika sherehe hiyo ya kiapo, ambapo wanaweza onyesha uaminifu wao kwa Australia, nakukubali wajibu na haki uraia wa Australia.
Soma kiapo kamili pamoja na taarifa zingine hapa.
Sherehe ya uraia

Takriban watu wapatao 100,000 hushiriki katika sherehe za uraia nchini Australia kila mwaka, wengi huchagua siku kuu ya Australia 26 Januari kama wakati na siku ya kula kiapo cha uraia.
Sherehe nyingi huandaliwa na halmashauri za jiji, kwa ujumla sherehe hizo huchukua muda wa saa moja hadi masaa mawili.
Huchukua kawaida kati ya wiki tatu na miezi sita kwa waliopita mtihani, hualikwa katika sherehe za uraia.

Watakao kuwa raia siku hiyo, wanastahili leta vitambulisho vyao.
“Wafanyakazi wa halmashauri ya jiji watatumia kitambulisho chako kulinganisha na majina kwenye orodha, watakapo ridhika kuwa mwenye kitambulisho yuko kwenye orodha, ndipo utaruhusiwa kuingia ndani ya ukumbi.” Kilner ameema.
"Watu wengi huja na leseni zoo za kuendesha gari au pasi za kusafiria."

Ruby Fowdar alisoma na kufanya kazi katika kanda ya Queensland kabla ya kupewa uraia.
“Sherehe yangu ya uraia ilikuwa kwenye siku kuu ya Australia."
“Ilikuwa wakati wa fahari, jina langu likiitwa na kupewa hati nikiambiwa wewe ni raia wa Australia, karibu katika jamii yetu kuanzia leo.”

Rasilimali za ziada:
Kwa taarifa ya ziada jinsi unavyoweza kuwa raia wa Australia, bofya hapa chini:
The Australia.gov.au Citizenship Guide
The Department of Home Affairs Citizenship Wizard
Kwa wanao hitaji msaada wa lugha, pigia simu shirika la ukalimani na tafsiri Translating and Interpreting Service (TIS) kwa namba hii 131 450.

