"Kuwa Urusi ni kama vile ndoto kuwa kweli kwa soka la Wairan.," Kocha wa Iran Carlos Queiroz alisema.
"Tumepata mafanikio haya kupitia kazi ngumu na kujitoa, kitu kilichoinua jinsi tunavyoheshimiwa na tunajisikia faraja kuwa hapa.
Iran itapiga kambi katika kituo cha mazoezi cha Lokomotiv Bakovka mjini Moscow. Hii itakuwa mara yao ya tano kuonekana kwenye fainali hizi za Kombe la Dunia.
Queiroz alisikika akisema, "Iran itakuwa na kikosi kizuri, na tutahakikisha kuindeleza ndoto kwa muda mrefu iwezekanavyo na tunatarajia kucheza sehemu yetu katika kufanya hili Kombe la Dunia kuwa bora milele."

Source: Getty
Timu hiyo ya Queiroz, inatarajiwa kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Lithuania mjini Moscow tarehe 8 mwezi huu wa sita na baadaye kuanza kampeini yao dhidi ya Morocco katika uwanja wa Mt Petersburg mnamo tarehe 15 mwezi huu.
Share

