Wakazi wa Gippsland huko kusini-mashariki mwa Victoria wamelazimika kukimbia makazi yao wakati moto mkubwa usiodhibitika ukitishia mali zao katika eneo hilo.
Siku ya Jumatatu asubuhi, moto ulikuwa ukiteketeza hekta 12,500 na utaendelea kuwa mkubwa, kwa mujibu wa Mtendaji Msaidizi wa Moto wa Misitu Chris Eagle.

Smouldering trees are seen in the Bunyip State Park, Victoria. Source: AAP
Alisema angalau miundombinu saba, ikiwa ni pamoja na nyumba, ziliathirika.
"Ilikuwa kama mvua ya majivu. Na ilisikika kama mvua juu ya paa, lakini si mvua ilikuwa ni majivu," Garfield mkazi wa Rhonda Simpson aliiambia SBS Habari baada ya kuokolewa.
"Ilikuwa kubwa sana na inatisha sana".
Moto katika kitongoji cha Bunyip Park, unawaka kilomita 65 mashariki mwa Melbourne, ulisababishwa na radi kali siku ya Ijumaa.

Smoke is seen in a tree line from a property in Gembrook, Victoria. Source: AAP
Onyo la dharura limeendelea kuwekwa kwa wakazi wa maeneo ya jirani, ikiwa ni pamoja na Budgeree, Budgeree Mashariki, Jeeralang, Jeeralang Junction, Jeeralang Kaskazini, Jumbuk, Yinnar na Yinnar Kusini. Bwana Eagle aliiambia ABC Habari kwamba bado siku kadhaa hadi moto huo kudhibitiwa.
Mwandishi wetu Frank Mtao, ataendelea kuwahafamisha hali inavyoendelea katika maeneo hayo, na kumbuka kufuatilia mtandao huu na kusikiliza vipindi vyetu vya habari.
Share

