Jacob Zuma ame jiuzulu rasmi kutoka wadhifa wake kama kiongozi wa Afrika Kusini. Tangazo laku jiuzulu kwake, lili tolewa katika hotuba kwa taifa iliyo peperushwa moja kwa moja.
Katika hotuba yake, Bw Zuma alisisitiza kuwa hatakama ame lazimishwa kujiuzulu, bado ana nia na ata endelea kuhudumia chama cha ANC.
Hotobua yake ime jiri pia baada ya kamati ya viongozi katika chama tawala African National Congress NEC, kusisitiza msimamo wao waku taka ajiuzulu.

Rais Jacob Zuma (kushoto) na Naibu Rais Cyril Ramaphosa katika mkutano wa serikali mjini in Cape Town. Source: AAP
Wanachama wa NEC walishiriki katika mikutano iliyo kamilika usiku wa maneno mara kadhaa, pamoja na kuwatuma wajumbe kuwasiliana na Bw Zuma kuhusu uamuzi wao. Imeripotiwa kuwa Bw Zuma alipuuza madai yote ambayo wajumbe hao wali wasilisha kwake.
Akikabiliwa kwa uwezekano wa muswada wakuto kuwa na imani kwa utenda kazi wake ambao ulikuwa uwasilishwe na chama chake cha ANC, Bw Zuma hakuwa na budi isipokuwa kujiuzulu kama alivyo shauriwa na chama chake.
Rais mpya wa Afrika Kusini anatarajiwa kutangazwa Ijumaa, wakati aliyekuwa naibu rais wa Bw Zuma, Cyril Ramaphosa anatarajiwa kuwa ndiye atakaye rithi wadhifa huo.
Share

