Marehemu Abe alipigwa risasi alipokuwa katika wilaya ya Nara, Japan kwenye kampeni ya uchaguzi. Anaye shukiwa kutekeleza mauaji hayo, alikamatwa mara moja na vyombo vya usalama katika eneo la tukio.

Maafisa wa usalama wamkamata mshukiwa wa shambulizi dhidi ya waziri mkuu wa zamani wa Japan Shinzo Abe. Source: The Asahi Shimbun via Getty Images
Imeripotiwa na mashirika ya habari kutoka Japan kuwa, Bw Abe alikimbizwa hospitalini kwa helikopta ambako, licha ya juhudi kubwa zamadaktari kifo cha Bw Abe kiliripotiwa masaa machache baadae.