Ofisi ya twakimu husamamia zoezi hilo nakuhesabu kila mtu aliye nchini katika usiku ulio tengwa kwa zoezi la sensa 2021.
Katika miaka ya nyuma Ofisi ya Takwimu ya Australia, iliwaajiri maelfu ya watu kukusanya data katika jamii katika usiku wa sensa 2021. Maafisa walio pewa jukumu laku kusanya data hizo, kutoka kila nyumba nchini kote mara nyingi walikuwa wakiwasaidia watu kufafanua maswali ambayo yamo ndani ya fomu za sensa 2021.

Afisa wa Ofisi ya Takwimu ya Australia akiwa na fomu za sensa Source: SBS
Ila janga la COVID-19 lili ilazimisha Ofisi ya Takwimu ya Australia, kuwekeza rasilimali za ziada katika tovuti yao ambako watu wenye ujuzi na uwezo wakutumia kompyuta na intanet, wali elekezwa kukamilisha zoezi la kujaza fomu za sensa 2021.

Mtu ajaza fomu ya sensa 2021 mtandaoni Source: ABS
Je! kwa wanachama wa jamii ambao hawana ujuzi wakutumia vifaa vyaki elektroniki, na ambao hawana uelewa wa Kiingereza walishirikije katika zoezi hilo ambalo ni lazima kila mtu ashiriki?
Bw Claude Muco ni afisa katika shirika la Illawarra Migrant Services mjini Wollongong, New South Wales. Alieleza Idhaa ya Kiswahili ya SBS kwamba shirika lake "lili zungumza na ofisi ya takwimu ya Australia, itoe uwekezaji wa ziada kwa mashirika yanayo toa huduma zakibinadam kwa jamii, ili ziwe na rasilimali zakutosha kuwasaidia wanachama wa jamii ambao wana matatizo yaku jaza fomu za sensa 2021 wenyewe."

Wanachama wa jamii wapewa msaada kujaza fomu za sensa 2021 Source: Getty
Bw Claude aliongezea kuwa "shirika lake pamoja na mashirika mengine yame wasiliana na mamlaka husika, kujadili uwezekano waku wahudumia watu wanao hitaji misaada yakushiriki katika zoezi la sensa 2021 katika ofisi zao au sehemu zingine maalum, vizuizi vya COVID-19 ndani ya jamii vikizingatiwa".