Baadhi yao hufanya mazoezi kwa sababu wame agizwa na wataalam wa afya, wengine kwa sababu hufurahia kufanya mazoezi mara kwa mara.

Sehemu zakufanyia mazoezi zilifungwa wakati wa kilele cha janga la UVIKO-19. Source: SBS
Wakati wa kilele cha janga la UVIKO-19, vizuizi ambavyo mamlaka waliweka kwa ajili yakudhibiti usambaaji wa virusi vya corona, vilifanya iwe vigumu kwa watu kuendelea kufanya mazoezi binafsi, na katika makundi kama ilivyokuwa mazoea yao.
Image
Katika mazungumzo na Idhaa ya Kiswahili ya SBS, Mwenyekiti wa Jamii yawatanzania wanao ishi jimboni NSW Frank Mtao alisema," Michezo ni mhimu kwa kuwasaidia watu kudumisha afya njema, michezo husaidia watu kupata marafiki pamoja na kuimarisha mahusiano kati ya watu na jamii mbali mbali.