Muhamasishaji wa itikadi za maisha ya Australia Justine Ruszczyk Damond alikuwa akipumua kwa tabu huku akipiga kelele wakati alpokuwa akipiga simu kwa namba ya dharura 911 kabla ya kupigwa risasi na polisi wa Marekani, kulingana na sauti ya simu.
Sauti mbili zilizorekodiwa za Bi Ruszczyk Damond kwenda kwa 911 zimeachiwa kwa umma Alhamis, wakati jaji wa Minneapolis alipoanza kuruhusu vizibiti kuonyeshwa katika kesi inayomuhusu Mohamed Noor.
Noor, mwenye umri wa miaka 33, alishtakiwa kwa mauji.
Bi Ruszczyk Damond, mwenye uraia pacha wa marekani na Australia, alipiga simu 911 kutoa taarifa juu ya uwezekano wa yeye kudhalilishwa kingono nyumbani kwakwe mnamo mwezi wa saba 2017.

Ex-police officer Mohamed Noor on May 1 before he was jailed over the fatal shooting of Justine Damond Ruszczyk . Source: AAP

Justine Damond Ruszczyk was shot dead by a police officer, after calling 911 about a possible sexual assault. Source: AAP
Katika simu ya kwanza, alisema, alisikika mwanamke aliyeonekana kuteseka na anafikiria alisikia sauti ikiomba "msaada".
Bi Ruszczyk Damond alipiga tena dakika nane baadae ili kuhakikisha polisi walipata anuani sawa. Akataarifiwa kuwa, polisi wako njiani.
Mkazi huyo wa zamani wa Sydney akaenda kukutana na gari ya polisi ndipo akapigwa risasi na Noor, ambaye alikuwa amekaa kiti cha abiria cha mbele.
Familia ya Bi Ruszczyk Damond walifungua mashtaka dhidi ya jiji la Minneapolis na wakafanikiwa kupewa kitita cha Dola za Kimarekani $US20 million sawa na Dola za australia ($A29 million) kama fidia.

John Ruszczyk (left), the father of Justine Damond Ruszczyk, with his wife Marian Hefferen. Source: AAP