Wawili hao hawaja pata fursa zaku tosha kucheza msimu huu kama ilivyo kuwa msimu ulio pita.
Bruce Kamau, 22, kwa mara nyingine atakuwa chini ya uongozi wa mkufunzi wa zamani wa Adelaide United na timu ya Australia ya wachezaji wa chini ya maika 23 Josep Gombau, ambaye chini ya uongozi wake, alikuwa mmoja wa nyota wakubwa wa soka katika A-League ambako alizua hisia mseto miongoni mwa walinzi alio kabiliana nao katika mechi. Image
Mchezo wa Kamau ulimfanya apendwe na mashabiki wengi wa Adelaide Utd, ambao aliwafurahisha zaidi, kwaku funga goli muhimu katika fainali ya A-League kabla ya kuhamia City mwaka wa 2016.
Josep Gombau pia alismsaidia Ruon Tongyik, 21, kuwa mlinzi mahiri ambaye huwa hasiti anapo kabiliana na washambuliaji wanao jaribu kuweka lango lake hatarini. Ruon alifaidi pia kupitia uongozi wa Gombau alipo chezea timu ya vijana wa Australia wenye umri wa miaka chini ya 23. Image
Bruce na Ruon wata kuwa wachezaji wa rasmi wa Wanderers mwisho wa msimu huu, ambako Gombau anaendelea na kazi yaku jenga upya timu aliyo rithi.
Share

