Waziri wa mambo ya ndani wa Kenya Fred Matiang’i, alithibitisha taarifa ambazo wakazi wa taifa hilo, walikuwa wakisubiri kupitia taarifa aliyo toa kwa vyombo vya habari.

Waziri wa mambo ya ndani wa Kenya Fred Matiang'i atoa taarifa kwa vyombo vya habari baada ya shambulizi laki gaidi katika hoteli ya DusitD2 mjini Nairobi,Kenya Source: AP
Taifa liko salama sasa na taifa lina endelea kuwa tulivu, wakenya na wageni wetu wote wako salama na wanastahili jihisi huru kuendelea kufanya shughuli zao kama kawaida. Tukumbuke sote kuwa, ugaidi hauta wahi tushinda, nasi kama taifa tuna endelea kuwa imara na hatuta jisalimisha wala kuogopa vitisho vya magaidi.
Imeripotiwa kuwa watu saba wamefariki, na mamlaka nchini humo wanatarajia idadi ya vifo kuongezeka uchunguzi unapo endelea baada ya shambulizi hilo la ugaidi. Ila familia zilizo fiwa, zime anza kuwazika wapendwa wao.

Wakenya washiriki katika mazishi ya walio uawa katika shambulizi lakigaidi katika hoteli ya DusitD2 Source: AP
Wanamgambo wa al-Shabab kutoka Somalia, hawaku kawia kudai shambulizi hilo, wakidai shambulizi hilo lilisababishwa na hatua ya rais wa marekani Trump, kuhamishia ubalozi wake mjini Jerusalem.
Wakati huo huo inspekta mkuu wa polisi ya Kenya, Boinnet amewaomba wakenya waendelee kuwa watulivu na wasichangie picha zozote, kutoka shambulizi hilo uchunguzi unapo endelea.
Share

