Mamia ya vituo vyaku piga kura vilifunguliwa mapema, hata hivyo wapiga kura wengi hawaku jitokeza kupiga kura, hali ambayo wengi wanalinganisha na wapiga kura kusalimu amri ya mrengo wa upinzani ulio waomba wafuasi wake kususia uchaguzi huo.
Idadi ya walio shiriki katika ngome za chama tawala katika marudio ya uchaguzi huo, ilikuwa ndogo kulinganisha na idadi ya walio shiriki katika uchaguzi ulio pita.
Wakati huo huo tume ya uchaguzi ya IEBC imetangaza kuwa, maeneo yanayo aminika kuwa ngome za mrengo wa upinzani yata pewa fursa yakupiga kura kesho Jumamosi 28 Oktoba 2017, kwa sababu ya uharibifu na vizuizi vilivyo wekwa katika sehemu zakupigia kura kwa mujibu wa tangazo toka kwa Ubalozi wa Kenya nchini Australia.
Hata hivyo, Rais Uhuru Kenyatta kwa sasa anaongoza katika hesabu za marudio ya uchaguzi huo, wakati matokeo ya mwisho yanatarajiwa muda usio mrefu.
Share

