Polisi New South Wales wamevunja maabara kubwa ya madawa ya kulevya huko Sydney kusini-magharibi na wamefanikiwa kukamata madawa ya kulevya yenye thamani ya milioni 5.2.
Mwanamume mwenye umri wa miaka 39 ameshtakiwa kwa makosa kadhaa ya madawa ya kulevya na amewekwa kizuizini baada ya kukataliwa dhamana.
Kamishna Msaidizi wa Polisi wa NSW Stuart Smith amesema, polisi wanachunguza ikiwa maabara ilitengeneza madawa ya kulevya ambayo yalisababisha vifo viwili kwenye tamasha la muziki la Defqon.1 mnamo Septemba.
Share

