Seneta huyo wa chama cha Libera Lucy Gichuhi, ameghaili kusudio lake pale alipotishia kutaja majina ya viongozi wenzake wanaodhihaki wenzao katika chama chao baada ya kuongea na Waziri Mkuu Scott Morrison.
Seneta huyo wa Australia Kusini, alitishia kutumia nafasi yake bungeni kutaja hadharani wenzake wenye tuhuma za kudhihaki na kunyanyasa wengine wakati wa patashika ya Uongozi wa chama hicho mwezi uliopita.
Lakini msemaji wa Seneta Gichuhi aliliambia shirika la habari la AAP kuwa, amemuachia Waziri Mkuu kulifanyia kazi swala hilo, hivyo hataweza kuwataja wanaotuhumiwa kudhihaki.
Share

