Ndege hiyo ya Indonesian ya shirika la ndege la Lion imeanguka muda mfupi tu baada ya kuondoka mji mkuu wa Jakarta, maafisa wa masuala ya anga walithibitisha leo jumatatu huku wakiongeza kuwa, utafutaji na uokoaji unaendelea hivi sasa.
Ndege JT-610 iliondoka kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Soekarno-Hatta Jakarta saa 6.21asb Jumatatu na ilikuwa ikiongozwa na Pangkal Pinang.
Ndege ilipotea karibu na Karawang katika jimbo la West Java.
"Imethibitishwa kuwa imeanguka," Yusuf Latif, msemaji wa Shirika la Taifa la Utafutaji na Uokoaji, alisema kwa ujumbe wa maandishi.
Msemaji wa kampuni ya uongozaji safari AirNav aliliambia shirika la utangazaji la Metro kuwa, ndege hiyo Boeing 737-800 ilipotea kwenye mawasiliano ya redio.
Msemaji wa shirika hilo la Lion Air Danang Mandala Prihantoro alinukuliwa akisema: "Tunaweza kuthibitisha kuwa, moja ya ndege zetu zimepotea kwenye mawasiliano na sehemu ilipo, haijulikani kwa sasa."
Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje aliliambia shirika la habari la SBS kuwa, itatutaarifu kama kuna Muastralia yoyote aliyeathirika kwa ajali hiyo.
Share

