Ndege ya shirika la ndege la Ethiopia ambayo ilianguka na kuua watu 157, ilikuwa ikitoa kelele ya ajabu huku ikifuatiwa na moshi mzito pamoja na mabaki yakimeguka ikiwa angani juu ya shamba la ng'ombe waliogopa, kabla ya kupiga ardhi, kulingana na mashahidi.
Ndege hiyo namba 302 iliondoka mji mkuu wa Ethiopia siku ya Jumapili asubuhi ikielekea Nairobi ikiwa na abiria kutoka nchi zaidi ya 30.
Wote waliokuwemo kwenye ndege hiyo Boeing 737 MAX-8 walifariki.
Rubani wa ndege hiyo, aliomba ruhusa ya kurudi, akisema alikuwa na matatizo - lakini ilikuwa tayari amechelewa.
Nusu ya mashahidi kadhaa waliohojiwa na Reuters katika mashamba ambapo ndege ilipoangukia, walisema, waliona moshi mzito, huku wanne wao walielezea kusikia mlio wa sauti kubwa.
"Ilikuwa ni mlio wa sauti ya kelele." Kama muanguko wa vyuma, alisema Turn Buzuna, mama wa nyumbani mwenye umri wa miaka 26 na mkulima ambaye anaishi mita 300 kutoka sehemu ndege hiyo ilipoangukia.
"Kila mtu anasema hawajawahi kusikia aina hiyo ya sauti kutoka kwenye ndege na ambayo iko chini ya njia yake."
Malka Galato, mkulima wa shayiri na ngano ambaye shamba lake ndipo ndege iliangukia ndani, pia alieleza kuona moshi na cheche nyuma ya ndege hiyo.
"Ndege ilikuwa karibu sana na ardhi na ikazunguka... Ng'ombe ambazo zilikuwa zinapata malisho shambani zilikimbia," alisema.
Tamirat Abera, mwenye umri wa miaka 25, alikuwa akitembea kwenye shamba wakati ule.

Photographs of the crew members of the Ethiopian Airlines flight ET 302 that crashed are displayed during a memorial service. Source: AAP
"Kulikuwa na moto na moshi mweupe ambao baadaye ukageuka mweusi," alisema
"Wakati ilipokuwa ikihaha angani, moto ulikuwa ukifuata mkia wake, kisha ikajaribu kuinua pua yake kupaa," mwingine Shahidi Gadisa Benti alisema.
"Baada ya kupita juu ya nyumba yetu, pua ilielekea chini na mkia uliinuka, ikaenda kupiga chini pua yake, kisha ikalipuka."
Mwezi Oktoba uliopita, muundo sawa wa ndege, unaoendeshwa na shirika la ndege la Lion, ilipata ajali nchini Indonesia, na kuua watu 189.
Uchina - ambao ni soko muhimu kwa Boeing - ikawa nchi ya kwanza kusimamisha ufanyaji kazi ndege hizo aina ya 737 MAX-8 siku ya Jumatatu. Ndege za Ethiopia zilifanya hivyo, wakisema uamuzi ulikuja kama "tahadhari ya ziada ya usalama."
Share

