Bi Gichuhi amechapisha tangazo akisema:
"Hesabu ya kura imethibitisha kwamba, mimi Lucy Gichuhi, nime chaguliwa kuwakilisha Kusini Australia ndani ya Seneti ya Australia".
Hesabu hiyo maalum ilifanywa na tume ya uchaguzi ya Australia Alhamisi mjini Adelaide.
"Nina heshima na shukrani kwa fursa yaku wahudumia wana Australia. Hii ni fursa yakutoa mchango wangu kwa taifa hili". "Sita zungumzia mchakato ambao umetufikisha hapa. Kama mwanasheria, nina heshimu mchakato waki sheria na uchaguzi" alisema. "Mimi ni raia wa Australia na nime fuzu kutoa huduma. Nita endelea kupokea ushauri kwa maswala haya yote tunapo endelea mbele.”
Hata hivyo chama cha Australian Labor (ALP) kime pinga uraia wake, swala hilo lita rejea katika mahakama kuu wiki ijayo, ambako uamuzi wa mwisho utatolewa kwa atakaye chukua nafasi ya Bw Day.
Share

