Maelfu wa tibua operesheni ya Idara ya ulinzi wa mipaka

Leo (Ijumaa28Agosti2015) Idara ya ulinzi wa mipaka ilitangaza kwamba maafisa wake watapiga doria wikiendi hii mjini Melbourne wakishirikiana na Polisi wa Victoria.

Waziri Mkuu wa Australia Tony Abbott akizungumza na afisa wa idara ya ulinzi wa mipaka.

Waziri Mkuu wa Australia Tony Abbott akizungumza na afisa wa idara ya ulinzi wa mipaka. Picha (AAP-Glenn Hunt) Source: AAP-Glenn Hunt

Lengo la operesheni hiyo ilikuwa kuzungumza na mtu yeyote ambaye maafisa hao wanakutana naye kuhakikisha ana visa/kibali halali cha kuwa nchini.

Ila dakika chache kabla maafisa wa Idara ya Ulinzi wa Mipaka na Polisi Victoria wazungumze na waandishi wa habari, mbele ya kituo kikuu cha treni cha Mtaa wa Flinders mjini Melbourne, maelfu ya waandamanaji walijumuika mbele ya kituo hicho kuonesha hasira yao dhidi ya oparesheni hiyo.
Waandamanaji waonesha hisia zao dhidi ya oparesheni ya idara ya ulinzi wa mipaka mjini Melbourne
Waandamanaji waonesha hisia zao dhidi ya oparesheni ya idara ya ulinzi wa mipaka mjini Melbourne Source: Picha: ABC News
Waandamanaji waliendelea kuongezeka katika eneo hilo na punde baadae walijumuika katikati ya barabara ambako magari na treni yalikabiliwa na kibarua chakuendelea na safari zao.

Taarifa hizo zilipo sambaa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, Idara ya ulinzi wa mipaka na Polisi wa Victoria walitangaza kwamba oparesheni hiyo imefutwa.

Hii hapa video fupi iliyorekodiwa na mtangazaji wa Idhaa ya SBS Punjabi.
'Refugees are welcome, border forces not'A group of 'anti-racism' activists stage a protest outside Flinders Street station against Australian government's alleged 'anti-refugee' policies. Posted by SBS Punjabi on Thursday, August 27, 2015


Je ulishuhudia/ulishiriki katika maandamano hayo? wasiliana nasi/tuma maoni yako hapa: swahili.program@sbs.com.au

 


Share

Published

Updated

By SBS SWAHILI
Source: SBS

Share this with family and friends


Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service