Dk. Magufuli ameapishwa jana Alhamis Novemba 5, 2020 katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma na Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma katika tukio lililoshuhudiwa na viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya nchi hiyo.
Katika kiapo chake , Rais Magufuli ameapa kuitetea, kuilinda na kuhifadhi Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na kuahidi kutumika kwa uaminifu katika kazi zake za Urais. "Uchaguzi sasa umekwisha, uchaguzi sasa umekwisha, uchaguzi sasa umekwisha" Ni kauli ya msisitizo kutoka kwa Rais John Pombe Magufuli, akihutubia baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.

Source: 2 Eyez Media
Amesema, jambo muhimu lililo mbele yao ni kuendeleza jitihada za kuijenga na kuiletea maendeleo Tanzania.Amesisitiza kuwa kiapo alichoapa yeye na Makamu wake Samia Suluhu watakienzi kwa nguvu zote, bila kujali tofauti za Kiitikadi, Kidini, Kikabila au Rangi na kueleza kuwa atashirikiana na Wananchi wote.
Magufuli alishinda kiti hicho cha Urais kwa kupata kura 12,516,252 ambayo ni asilimia 84 ya kura zote zilizopigwa. Tundu Lissu kutoka chama cha upinzani cha Chadema alishika nafasi ya pili kwa kupata kura 1,933,271 ya kura zote ziizopigwa.