Kwa maoni ya mahakama ya upeo, kesi tisa zalizizo wasilishwa ndani ya mahakama hiyo zilikuwa na hoja sawa.
Hakimu Mkuu wa Kenya Bi Martha Koome, alisoma mukhtasari wa uamuzi wa Mahakama ya Upeo nakutoa sababu za kila uamuzi ambao mahakama hiyo ilifikia. Mahakama ya Upeo imeridhika kuwa, hakuna ushahidi wakutosha kuwa tume huru ya uchaguzi ya Kenya (IEBC), haikutekeleza wajibu wake kikatiba. Kwa hiyo hakuna sababu ya mahakama hiyo kubatilisha ushindi wa Dr William Ruto.
Dr Ruto hajawahi poteza uchaguzi wowote alio wania katika maisha yake yakisiasa. Kufuatia uamuzi wa mahakama ya upeo, Dr William Ruto ata apishwa rasmi kuwa Rais wa tano wa Kenya tarehe 13 Septemba 2022.