Malkia Elizabeth ll alirithi wadhifa huo akiwa na miaka 25, punde baada ya babake kuaga dunia. Wakati huo Malkia Elizabeth ll alikuwa katika ziara nchini Kenya katika hoteli ya Treetops ambayo ilikuwa katika mbuga yakitaifa ya Aberdare pamoja na mumewe Prince Philip.
Miezi michache baada yakuwa Malkia, waafrika walipigwa marufuku kuingia katika kanda nzima ya Aberdares, na amri ilitolewa kwa wanajeshi wawapige risasi waafrika wakiwaona katika eneo hilo. Ina aminika kuwa wapiganaji wa uhuru wa Mau Mau, waliteketeza kwa moto hoteli ya Treetops 27 Mei 1954.
Malkia Elizabeth ll ame aga dunia akiwa na miaka 96. Mwanawe wa kwanza Prince Charles atarithi kiti chake cha enzi, nakupewa cheo cha Mfalme wa Uingereza pamoja na nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola.