Mtu huyo mwenye umri wa takribani miaka 40 hivi, aliyekuwa amevalia vazi aina ya 'tracksuit', kofia na glavu za mikononi zilizoacha vidole vyake wazi, alipanda daraja hilo majira ya saa 10:30 alfajiri ya leo hii Jumatano.
Ila baada ya saa 3:30 asubuhi, alijisalimisha kwa wana usalama na akashuka toka juu kuelekea kilipo kikosi cha uokoaji cha Polisi ambao walimfunga pingu na kumshusha chini.
"Tunaweza kuthibitisha kuwa, mtu huyo yuko salama chini ya ulinzi wa Polisi," Polisi NSW ilisema kupitia mtandao wa tweeter.
Aliwekwa kwenye machela na kuchukuliwa na gari ya wagonjwa ya kikosi cha huduma ya kwanza.
Foleni za magari zilikithiri wakati wa tukio hilo, kwani iliwapasa maafisa usalama kufunga baadhi ya barabara wakati wakiwa wanafanya mazungumzo na mtu huyo.
Ilipofika mida ya saa 2 asubuhi, foleni ya magari kupita darajani hapo ilikuwa kubwa kwa zaidi ya kilomita 15 kwa pande zote mbili hasa file za kuingia mjini.
Mabasi kupita darajani hapo, yalicheleweshwa kwa zaidi ya nusu saa lakini treni zilikuwa zikipita kama kawaida.
Si ruhusa kupanda daraja la Sydney Harbour isipokuwa kwa kibali maalumu na anayekamatwa kwa tukio hilo, anaweza kupigwa faini $3000.
Share

